Tanzania; Leo tarehe 25/07/2024, serikali kupitia Wizara ya Elimu wametangaza nafasi za mafunzo ya ualimu wa shule za msingi. Hivyo, Huu ni Mwongozo wa Mfumo wa Maombi ya Mafunzo ya Ualimu 2024/2025. Mwongozo huu unalenga kuwapa watumiaji maelezo kamili kuhusu jinsi ya kutumia Mfumo wa Udahili na Usimamizi wa Vyuo vya Ualimu (TCMS) kwa ufanisi. Imeundwa kwa ajili ya watumiaji wote wa mfumo, wakiwemo wasimamizi wa vyuo, wafanyakazi wa udahili, wanafunzi Pamoja na Wafanyakazi makao makuu ya wizara.
Lengo kuu la mwongozo huu ni kuongoza mtumiaji hatua kwa hatua katika kila kipengele cha mfumo, kuanzia mwanafunzi anapoomba chuo, usajili na kuingia hadi usimamizi wa wanafunzi, masomo, na taarifa. Mwongozo huu unaelezea kwa kina kazi zote muhimu za mfumo, unatoa maelekezo ya wazi na mafupi, na unajumuisha picha za skrini na michoro ili kuifanya iwe rahisi kuelewa namana ya kutumia mfumo huu.
Mfumo wa Maombi ya Mafunzo ya Ualimu 2024
Malengo makuu ya mwongozo huu, kuboresha mchakato wa udahili na kuongeza ufanisi katika usimamizi wa vyuo vya ualimu. Tunatumai mwongozo huu utakuwa rasilimali muhimu kwa watumiaji wote wa Mfumo wa Udahili na Usimamizi wa Vyuo vya Ualimu. Tunawahimiza watumiaji kusoma mwongozo huu kwa makini na kufuata maelekezo kwa uangalifu ili kuhakikisha matumizi bora ya mfumo. Ikiwa watumiaji watakumbana na matatizo yoyote au maswali, wanaweza kuwasiliana na timu ya usaidizi wa mfumo kwa usaidizi. Kwa kutumia mwongozo huu, watumiaji wataweza:
- Kuelewa vyema madhumuni na utendaji wa Mfumo wa Udahili na Usimamizi wa Vyuo vya Ualimu.
- Kuelewa namna ya kutuma maombi ya kujiunga na vyuo vya ualimu kwa wanafunzi na waombajii
- Kujifunza jinsi ya kujisajili na kuingia kwenye mfumo.
- Kudhibiti mchakato wa udahili wa wanafunzi, kuanzia kupokea maombi hadi kutoa barua za uandikishaji.
- Kuendesha masuala ya wanafunzi, kama vile usajili wa kozi, malipo ya ada, na ufuatiliaji wa mahudhurio.
- Kudhibiti mipango ya masomo, kozi, na ratiba za masomo.
- Kuunda na kutoa ripoti mbalimbali kuhusu wanafunzi, masomo, na shughuli za chuo.
- Kutatua matatizo ya kawaida yanayoweza kutokea wakati wa kutumia mfumo.
Watumiaji wa Mwongozo
Mwongozo huu utatumika na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia pamoja na Watumishi katika vyuo vya ualimu kupitia moduli mbalimbali za mfumo. Pia mfumo utatumika na wanafunzi watakaokuwa wanataka kujiunga na vyuo vya Ualimu katika kozi mbalimbali kwa ajili ya kufanya udahili, usajili na kuona maendelkeo ya kitaaluma.
Mpangilio wa Mwongozo
Mwongozo wa Mfumo wa Mfumo wa Udahili na Usimamizi vyuo vya ualimu chini ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia una Sehemu kuu tatu (3) ambazo ni Sehemu ya kwanza ya utangulizi; Sehemu ya pili ni Mfumo wa Upande wa Mwombaji (Front office); Sehemu ya tatu ni Upande wa Viongozi (Back Office) na Hitimisho la Mwongozo.
Bonyeza hapa kudownload mwongozo wa mfumo wa maombi ya mafunzo ya Ualimu
Huu mwongozo unapatikana katika tovuti ya Wizara ya Elimu Tanzania
AINA YA MAFUNZO (KOZI)
Stashahada Maalumu ya Ualimu Elimu ya Msingi katika masomo ya Sayansi na Hisabati (Miaka 03)
VYUO VINAVYOTOA MAFUNZO: Monduli, Butimba, Klerruu, Songea, Tukuyu, Kasulu, Mpwapwa, Morogoro, Korogwe naTabora.