Leo kutoka Utumishi (PSRS), Wametangaza Ajira mpya za ualimu, nafasi za kazi za walimu, Nafasi za Ajira za Ualimu Utumishi – Ajira za Walimu 2025; Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma kwa niaba ya Sekretarieti za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa anakaribisha maombi ya kazi kutoka kwa Watanzania wenye sifa na uwezo wa kujaza nafasi 11,015 kama ilivyoainishwa katika tangazo hili.
Ajira Portal chaneli | Jiunge hapa |

Ajira Mpya za Walimu 2025
1. Mwalimu daraja la IIIA – Nafasi 2851
2. Mwalimu daraja la IIIA – Elimu ya Awali – Nafasi 20
3. Mwalimu daraja la IIIA – Elimu Maalum – Nafasi 13
4. Mwalimu daraja la IIIB – Shule ya Msingi – Nafasi 464
5. Mwalimu daraja la IIIB – Elimu ya Awali – Nafasi 15
6. Mwalimu daraja la IIIB – Elimu Maalum – Nafasi 7
7. Mwalimu daraja la IIIB – Kemia, Nafasi 488
8. Mwalimu daraja la IIIB – Fizikia, Nafasi 740
9. Mwalimu daraja la IIIB – Hisabati, Nafasi 663
10. Mwalimu daraja la IIIB – Biolojia, Nafasi 505
11. Mwalimu daraja la IIIB – Jiografia, Nafasi 175
12. Mwalimu daraja la IIIB – Kiingereza, Nafasi 390
13. Mwalimu daraja la IIIB – Fasihi ya Kiingereza, Nafasi 65
14. Mwalimu daraja la IIIB – Kiswahili, Nafasi 142
15. Mwalimu daraja la IIIB – Historia, Nafasi 152
16. Mwalimu daraja la IIIB – Uraia, Nafasi 59
17. Mwalimu daraja la IIIB – Tehama, Nafasi 59
18. Mwalimu daraja la IIIB – Somo la Biashara, Nafasi 24
Nafasi ni nyingi sana hii hapo juu ni orodha fupi tafadhali gusa hapo chini kuona nafasi zote.
Bonyeza hapa kudownload Tangazo la nafasi za kazi za Ualimu 2025
Endelea na baadhi ya maelezo chini hapo.
Ajira Mpya za Walimu 2025 Utumishi.
Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania wenye umri usiozidi miaka 45 isipokuwa kwa wale tu walioko kazini serikalini.
Waombaji wa nafasi za Mwalimu Daraja la III B na Mwalimu Daraja la III C wahakikishe wanambatisha HATI YA MATOKEO (ACADEMIC TRANSCRIPT) katika mfumo wa “Ajira Portal” kwa ajii ya utambuzi wa masomo ya kufundishia.
Waombaji wote waambatishe cheti cha kuzaliwa kilichothibitishwa na Mwanasheria/Wakili.
Ajira za Walimu (UALIMU) 2025 Utumishi – Nafasi 11015 za Ualimu
Waombaji ambao tayari ni watumishi wa Umma na wamejipatia sifa za kuingilia katika kada tofauti na walizonazo, wapitishe barua zao za maombi ya nafasi za kazi kwa Waajiri wao na Waajiri wajiridhishe ipasavyo.
Waombaji waambatishe maelezo binafsi yanayojitosheleza (Detailed C.V) yenye anwani na namba za simu za kuaminika pamoja na majina ya wadhamini (referees) watatu wa kuaminika.
Maombi yote yaambatane na vyeti vya taaluma, maelezo, nakala za vyeti 44 vilivyothibitishwa na Mwanasheria/Wakili ambavyo ni vyeti vya kuzaliwa, kidato cha Nne, kidato cha Sita kwa wale waliofikia kiwango hicho, na vyeti vya kuhitimu mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi husika.
Jinsi ya kutuma maombi katika nafasi za Ajira za Walimu 2025 kutoka Utumishi.
Mwisho wa kutuma maombi ya kazi ni tarehe 02 Agosti, 2024.
MUHIMU: Kumbuka kuambatisha barua yako ya maombi ya kazi iliyosainiwa
pamojana vyeti vya elimu, anuani ya barua hiyo ielekezwe kwa;
KATIBU,
OFISI YA RAIS,
SEKRETARIETI YA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA UMMA,
S. L. P. 2320, DODOMA.
Maombi yote yatumwe kwenye mfumo wa kielektroniki wa Ajira (Recruitment 45 Portal) kupitia anuani ifuatayo; https://portal.ajira.go.tz (Anuani hii pia inapatikana kwenye tovuti ya Sektretarieti ya Ajira kwa kuingia sehemu iliyoandikwa‘Recruitment Portal’) (Anuani hii pia inapatikana kwenye tovuti ya Sektretarieti ya Ajira kwa kuingia sehemu iliyoandikwa‘Recruitment Portal’)