Leo Julai 30, 2024 JWTZ Wametangaza Nafasi za Jeshi JWTZ 2024 – Ajira Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ). Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) linatangaza nafasi za kuandikishwa Jeshini kwa vijana wa kitanza nchi wenye elimu ya kidato cha nne na kidato cha sita. Aidha, uandikishwaji utahusisha vijana walopko katika makambi ya Jeshi la Kujenga Taifa ‘Operesheni General Venance Mabeyo’ na walioimaliza makambi ambao wamefanya mafunzo ya JKT kwa Mujibu wa Sheria na kwa Mkataba wa kujitolea.
Nafasi za Jeshi JWTZ
SIFA ZA MWOMBAJI (VIJANA WALIOPO JKT NA WALIOIMALIZA MKATABA WA JKT)
Vijana wenye nia ya kuandikishwa Jeshi wanatakikwa kuwa na sifa zifuatazo:-
- Awe raia wa Tanzania.
- Awe na umri usiozidi miaka 25.
- Awe na afya nzuri na akili timamu.
- Mwenye tabia na nidhamu nzuri, hajapakiatana na hatia ya makosa ya jinai mahakamani na kufungwa.
- Awe na cheti halisi cha kuzaliwa.
- Awe na vyeti vya shule.
- Awe hajatumikia Jeshi la Polisi, Magereza, Chuo cha Mafunzo au Kikosi Maalumu cha kuzuia Magendo.
- Awe amehitimu mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa kwa Mkataba wa kujitolea miaka miwili (2) au mafunzo ya Mujibu wa Sheria na kutunukiwa cheti.
Ajira Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ)
Bonyeza hapa kudownload tangazo la nafasi JWTZ
Endelea kusoma maelezo mengine kwa chini..
Nafasi za Jeshini 2024 – Nafasi za kujiunga na Jeshi 2024 JWTZ
UTARATIBU WA KUTUMA MAOMBI JESHINI (JWTZ)
Utaratibu wa kutuma maombi ni ufuatao:-
a. Kwa vijana waliopo katika makambi ya JKT ‘Operesheni General Venance Mabeyo’ taratibu zao zitatainishwa na Makao Makuu ya Jeshi.
b. Kwa vijana waliohitimu mafunzo ya Makambi ya JKT, maombi yao yaandikwe kwa mkono na kuwasilishwa Makao Makuu ya Jeshi Dodoma kuanzia tarehe 01 Agosti, 2024 hadi tarehe 14 Agosti, 2024 wakiwa na vivuli vya nyaraka zifuatazo:-
(1) Nakala ya kitambulisho cha Taifa au namba ya NIDA.
(2) Nakala ya cheti cha kuzaliwa.
(3) Nakala za vyeti vya shule.
(4) Nakala ya cheti cha JKT.
(5) Picha nne (4) za rangi ya ukubwa wa pasipoti.
Ajira Mpya Jeshini – Nafasi za kazi Jeshi la JWTZ 2024
MAOMBI YATUMWE KWA ANUANI IFUATAYO
Mkuu wa Utumishi Jeshini,
Makao Makuu ya Jeshi,
Sanduku la Posta 194,
DODOMA, Tanzania