Leo kutoka Utumishi (PSRS), Tangazo la ajira mpya, Nafasi za kazi Mkinga – Utumishi Julai 2024; Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkinga amepokea kibali cha Ajira mpya kwa ikama ya mwaka 2023/2024 kutoka kwa Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora chenye Kumb.Na.FA.97/288/01/09 cha tarehe 25/06/2024. Hivyo Watanzania wote wenye sifa wanatangaziwa kutuma maombi ya kazi kwa nafasi zifuatazo:-
Kumb. Na. HW/MKG/S.85/20/137
Ajira Mpya Mkinga
1. DEREVA II – NAFASI 05
- Kufanya matengenezo madogo madogo ya gari.
2. WANDISHI MWENDESHA OFISI II – NAFASI 02
- Kutafuta majalada na nyaraka zinazohitajika katika utekelezaji wa majukumu ya kazi
3. MSAIDIZI WA KUMBUKUMBU DARAJA II – NAFASI 03
- Kufuatilia mzunguko wa majalada ndani na nje ya Taasisi
4. MTENDAJI WA KIJIJI DARAJA III – NAFASI 02
- Kusimamia, kukusanya na kuhifadhi kumbukumbu zote na nyaraka za kijiji;
Bonyeza hapa kudownload tangazo la nafasi za kazi Mkinga
Endelea kusoma maelezo mengine sehemu ya chini hapa…
Ajira Mpya Halmashauri ya wilaya ya Mkinga.
Waombaji kazi ambao tayari ni waajiriwa katika nafasi za kuingilia walioko katika Utumishi wa Umma wasiombe na wanatakiwa kuzingatia maelekezo yaliyo katika Waraka Na. CAC.45/257/01/D/140 wa tarehe 30 Novemba, 2010.
Mwisho wa kutuma maombi ya kazi ni tarehe 31 Julai, 2024.
MUHIMU: Kumbuka kuambatisha barua yako ya maombi ya kazi iliyosainiwa pamoja
na vyeti vya elimu, anuani ya barua hiyo ielekezwe kwa: –
Mkurugenzi Mtendaji,
Halmashauri ya Wilaya Mkinga,
S.L.P. 6005,
TANGA.