Leo kutoka sekretarieti ya ajira (PSRS), Pitia tangazo la ajira mpya katika Nafasi za Kazi Wilaya ya Ruagwa – Utumishi Julai 2024. Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa amepokea kibali cha Ajira mpya kwa ikama ya mwaka 2023/2024 kutoka kwa Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora chenye Kumb.Na.FA.97/288/01/09 cha tarehe 25/06/2024. Hivyo Watanzania wote wenye sifa wanatangaziwa kutuma maombi ya kazi kwa nafasi zifuatazo:
Ajira Mpya Ruangwa
1. DEREVA DARAJA II – NAFASI 6
2. MWANDISHI MWENDESHA OFISI DARAJA LA II – NAFASI 5
3. MSAIDIZI WA KUMBUKUMBU DARAJA LA II – NAFASI 4
4. MTENDAJI WA KIJIJI DARAJA LA III – NAFASI 4
Ajira Mpya Ruangwa 2024
Mwisho wa kutuma maombi ya kazi ni tarehe 08 Agosti, 2024
MUHIMU: Kumbuka kuambatanisha barua yako ya maombi ya kazi iliyosainiwa pamoja na vyeti vya elimu, anuani ya barua hiyo ielekezwe kwa:-
MKURUGENZI MTENDAJI,
HALMASHAURI YA WILAYA YA RUANGWA,
15 BARABARA YA BOMA,
S. L. P 51,
RUANGWA, LINDI.