Leo tarehe 23/07/2024 kutoka Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Mufindi anawatangazia Watanzania wenye sifa na nia ya kufanya kazi katika Halmashauri ya Wilaya Mufindi kuomba nafasi ya kazi iliyotajwa hapo chini, baada ya kupokea kibali chenye Kumb.Na. FA. 97/288/01/09 cha tarehe 25 Juni, 2024 na kibali cha ajira mbadala chenye Kumb. Na. FA. 228/613/01/C/068 cha tarehe 12 Juni 2024 kutoka kwa Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora.
Ajira Mpya Mufindi
1. MSAIDIZI WA KUMBUKUMBU DARAJA LA II – NAFASI 5
2. MTENDAJI WA KIJIJI DARAJA LA III – NAFASI 13
Bonyeza hapa kudownload pdf ya tangazo la nafasi za kazi Mufindi
Endelea kusoma maelezo mengine zaidi hapa chini.
AJIRA MPYA MUFINDI – NAFASI ZA HALMASHAURI 2024.
Mwisho wa kutuma maombi ya kazi ni tarehe 04/08/2024
MUHIMU: Kumbuka kuambatisha barua yako ya maombi ya kazi iliyosainiwa pamoja na vyeti vya Elimu, aidha anuani ya barua hiyo ielekezwe kwa:
Mkurugenzi Mtendaji,
Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi,
S.L.P 223,
MAFINGA.