Leo 26/07/2024, Sekretarieti ya Ajira Serikalini imetangaza ajira mpya katika Nafasi za Kazi Wilaya ya Iramba – Utumishi Julai 2024. Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba amepokea kibali cha Ajira mpya kwa ikama ya mwaka 2023/2024 kutoka kwa Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora chenye Kumb.Na.FA.97/288/01/09 cha tarehe 25/06/2024 pamoja na Kibali cha Ajira Mbadala chenye Kumb Na.FA.228/613/01/D/022 cha tarehe 21 Juni,2024 kwa mchanganuo ufuatao: –
Ajira Mpya Iramba
1. MTENDAJI WA KIJIJI DARAJA LA III –NAFASI (5)
2. MWANDISHI MWENDESHA OFISI II -– NAFASI 4
3. MSAIDIZI WA KUMBUKUMBU DARAJA LA II – NAFASI 4
4. DEREVA DARAJA LA II – NAFASI 3
Maombi yote yaambatane na vyeti vya Elimu na Taaluma vilivyothibitishwa na Mwanasheria/Wakili ambavyo ni vyeti vya Kidato cha Nne au Sita kwa wale waliofikia kiwango hicho na vyeti vya kuhitimu mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi husika.
Ajira Mpya Iramba 2024
Mwisho wa kutuma maombi ya kazi ni tarehe 8 Agosti, 2024.
MUHIMU: Kumbuka kuambatisha barua yako ya maombi ya kazi iliyosainiwa pamoja na vyeti vya elimu, anuani ya barua hiyo ielekezwe kwa: –
Mkurugenzi Mtendaji,
Halmashauri ya Wilaya Iramba,
S.L.P. 355,
Kiomboi-Iramba.