Ajira mpya, Nafasi za kazi Wilaya ya Morogoro – Utumishi; Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro amepokea kibali cha Ajira chenye Kumb. Na. FA.97/288/01/09 cha tarehe 25/06/2024 kutoka kwa Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora. Hivyo Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro anatangaza nafasi za kazi na anakaribisha maombi kwa Watanzania wenye sifa za kujaza nafasi hizo kama ifuatavyo:-
Nafasi zilizo tangazwa Morogoro
- MSAIDIZI WA KUMBUKUMBU DARAJA II – NAFASI 02
- DEREVA DARAJA II – NAFASI 05
- MTENDAJI WA KIJIJI DARAJA III – NAFASI 10
Bonyeza hapa kutuma maombi https://portal.ajira.go.tz/advert/index katika mfumo wa ajira utumishi.
Endelea kusoma maelezo chini..
Ajira Mpya Wilaya ya Morogoro
Mwisho wa kutuma maombi ya kazi ni tarehe 29 Julai, 2024.
MUHIMU: Kumbuka kuambatanisha barua yako ya maombi ya kazi iliyosainiwa na
ielekezwe kwa anuani ya;-
Mkurugenzi Mtendaji,
Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro,
S.L.P 1880,
MOROGORO