leo Wizara ya Elimu Tanzania wametatoa TANGAZO LA NAFASI ZA MAFUNZO YA UALIMU NGAZI YA STASHAHADA YA UALIMU ELIMU YA AWALI NA MSINGI KWA MWAKA WA MASOMO 2024/2025
Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia anatangaza nafasi za mafunzo ya Ualimu ya Stashahada ya Ualimu Elimu ya Awali na Msingi. Mafunzo yatakayotolewa ni Stashahada ya Ualimu Elimu ya Awali na Msingi (Miaka 02) na Stashahada Maalumu ya Ualimu Elimu ya Msingi (Miaka 03) katika masomo ya sayansi na hisabati. Waombaji wa mafunzo ya Ualimu ya Stashahada ya Ualimu Elimu ya Awali na Msingi (miaka 02) ni wahitimu wa Kidato cha sita wenye ufaulu wa Daraja la Kwanza hadi la Tatu (I-III).
Mafunzo ya Ualimu 2024
Waombaji wa mafunzo ya Ualimu ya Stashahada Maalumu ya Ualimu Elimu ya Msingi (Miaka 03) katika masomo ya sayansi na hisabati ni wahitimu wa kidato cha nne wenye ufaulu wa Daraja la kwanza hadi la tatu (I-III). Mafunzo haya yatatolewa katika vyuo vya Serikali na Vyuo visivyo vya Serikali. Vyuo vya ualimu visivyo vya Serikali vitatoa mafunzo haya baada ya kuwasilisha maombi na kupata kibali cha Kamishna wa Elimu. Wizara inakaribisha maombi ya kujiunga na mafunzo ya Ualimu katika Vyuo vya Serikali na visivyo vya Serikali kwa kuzingatia sifa zilizobainishwa katika tangazo hili.
AINA YA MAFUNZO NA VYUO VINAVYOTOA MAFUNZO YA UALIMU 2024
Stashahada ya Ualimu Elimu ya Msingi mchepuo wa Sayansi ya Jamii (kwa kutumia lugha ya kiswahili) – Mhonda, Murutunguru na Vikindu
Stashahada ya Ualimu Elimu ya Msingi mchepuo wa Sayansi ya Jamii (kwa kutumia lugha ya kingereza) – Mpuguso na Shinyanga
Stashahada ya Ualimu Elimu ya Msingi mchepuo wa Sayansi ya jamii na lugha ya kiswahili (kwa kutumia lugha ya kiswahili). – Bunda naTandala