Kama wewe ni mwomba ajira katika Sekretarieti ya Ajira katika OR-Utumishi wa Umma, Basi hizi ndizo Sifa za Afisa Sheria Katika Ajira Utumishi.
Afisa Sheria ni mtaalamu mwenye mafunzo na utaalamu katika sheria, ambaye hufanya kazi katika taasisi za kiserikali, mashirika binafsi, au kampuni. Majukumu yake kuu ni kutoa ushauri wa kisheria, kuandaa na kupitia mikataba, na kuhakikisha kuwa shughuli za taasisi zinaendeshwa kwa mujibu wa sheria na kanuni. Afisa Sheria pia huwakilisha taasisi au wateja wake mahakamani na katika mashauri mengine ya kisheria.
Aidha, Afisa Sheria anahusika na kusimamia masuala yote ya kisheria ndani ya taasisi, ikiwa ni pamoja na kutatua migogoro, kushughulikia masuala ya ajira na utawala, na kutoa mafunzo kwa wafanyakazi kuhusu sheria zinazohusiana na kazi zao. Hivyo, nafasi ya Afisa Sheria ni muhimu sana katika kulinda maslahi ya taasisi na kuhakikisha uwajibikaji wa kisheria.
Sifa: Kuajiriwa wenye Shahada ya kwanza ya Sheria kutoka Vyuo vinavyotambuliwa na Serikali waliomaliza mafunzo ya uwakili yanayotambuliwa na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali.
Mshahara wa Afisa Sheria 2024/2025
Ni upi mshahara wa mtu aliesomea Maswala ya Sheria au Uanasheria?
Ngazi ya mshahara ni TGS. E yaani Tshs. .690000.00 na kuendelea kwa kila mwezi.