Kama wewe ni mwomba ajira katika Sekretarieti ya Ajira katika OR-Utumishi wa Umma, Basi hizi ndizo Sifa za Usimamizi wa data za kierektroniki (Database Administration) Katika Ajira Utumishi.
Msimamizi wa Hifadhidata (Database Administrator) ni mtaalamu anayehusika na kusimamia, kudumisha, na kulinda hifadhidata ya shirika au kampuni. Majukumu yao yanajumuisha kuhakikisha hifadhidata inapatikana wakati wote, kufanya maboresho ya utendaji, na kuhakikisha usalama wa data dhidi ya vitisho kama udukuzi na uharibifu. Pia, wanajibika kwa kutekeleza sera za usalama wa data, kufanya chelezo za mara kwa mara, na kurejesha data pale inapohitajika.
Msimamizi wa Hifadhidata pia anashirikiana na timu nyingine kama vile waendelezaji wa programu na wachambuzi wa mifumo ili kuhakikisha hifadhidata inakidhi mahitaji ya kibiashara na kiteknolojia ya shirika. Wanaweza pia kufanya kazi ya kubuni hifadhidata mpya na kushauri kuhusu teknolojia bora za kuhifadhi na kusimamia data. Kwa ujumla, wanachangia katika kuhakikisha taarifa muhimu za shirika zinapatikana, zinahifadhiwa kwa usalama, na zinaweza kutumika kwa ufanisi.
Sifa: Kuajiriwa wenye Stashahada ya Juu au Shahada ya kwanza ya Kompyuta katika moja ya fani zifuatazo; Sayansi ya Kompyuta, Teknolojia ya Habari, Teknolojia ya Habari na Mawasiliano, Menejimenti ya Mifumo ya Habari.
Viwango vya mishahara endelea kwa chini.
Mshahara wa Msimamizi wa Hifadhidata (Database Administrator) 2024/2025
Ni upi mshahara wa mtu aliesomea Maswala ya Database Administration?
Ngazi ya mshahara ni TGS B yaani Tshs. 690,000.00 na kuendelea kwa kila mwezi.