Kama wewe ni mwomba ajira katika Sekretarieti ya Ajira katika OR-Utumishi wa Umma, Basi hizi ndizo Sifa za Fundi Sanifu (Umeme) Katika Ajira Utumishi.
Fundi Sanifu (Umeme) ni mtaalamu anayehusika na ufungaji, matengenezo, na ukarabati wa mifumo ya umeme katika majengo, viwanda, na maeneo mengine yanayohitaji umeme. Anahakikisha kuwa mifumo ya umeme inafanya kazi ipasavyo kwa kufuata kanuni za usalama na viwango vilivyowekwa. Aidha, fundi sanifu anaweza kushughulika na usakinishaji wa vifaa vya umeme, kubaini hitilafu, na kuzirekebisha kwa ufanisi ili kuhakikisha matumizi bora ya nishati na kuepuka ajali za umeme.
Kazi ya fundi sanifu inahitaji ujuzi maalum wa kusoma ramani za umeme, kutumia vifaa vya kipimo, na kuelewa teknolojia za kisasa za umeme. Katika nafasi hii, fundi sanifu anahitajika kuwa na uelewa mzuri wa usalama wa umeme na uwezo wa kufanya kazi kwa ushirikiano na timu nyingine za kiufundi ili kuhakikisha miradi inakamilika kwa wakati na kwa ubora unaotakiwa.
Kuajiriwa wenye mojawapo ya sifa zilizotajwa hapa chini;
- Waliohitimu kidato cha sita (VI) na kufuzu mafunzo ya ufundi wa miaka miwili kutoka Chuo kinachotambuliwa na Serikali katika fani ya umeme,
- Waliohitimu kidato cha nne (IV) na kufuzu kozi ya ufundi ya miaka mitatu kutoka Vyuo vya Ufundi vinavyotambuliwa na Serikali katika fani ya umeme,
- Wenye Cheti cha Majaribio ya Ufundi Hatua ya I kutoka Chuo cha Ufundi kinachotambuliwa na Serikali; na
- Wenye Stashahada ya Kawaida katika fani ya umeme kutoka Chuo kinachotambuliwa na Serikali.
Kiwango cha mshahara endelea sehemu ya chini.
Mshahara wa Fundi Sanifu (Umeme) 2024
Ni upi mshahara wa mtu aliesomea Maswala ya Fundi Sanifu (Umeme)?
Ngazi ya mshahara ni TGS C yaani Tshs. 350,000.00 mpaka 490,000.00 na kuendelea kwa kila mwezi. Hii hulipwa kwa kulingana na Elimu.