Vigezo vya kupata Mkopo kutoka HESLB Bodi ya Mikopo Tanzania sifa za jumla zinamtaka mwombaji mkopo atimize masharti yafuatayo: –
- Awe Mtanzania;
- Awe ameomba mkopo kupitia mfumo wa maombi ya mkopo (OLAMS);
- Awe amedahiliwa katika taasisi ya elimu ya juu yenye ithibati, kwa muda wote (full time) isipokuwa wanafunzi wanaodahiliwa kusoma katika Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (Open University of Tanzania);
- Asiwe na ufadhili mwingine kwa masomo yake ya elimu ya juu;
- Kwa waombaji wa shahada ya kwanza, asiwe ameajiriwa na serikali au na sekta binafsi
- Mwanafunzi anayeendelea na masomo anayeomba mkopo mwenye matokeo/ripoti za matokeo zinazoonesha ufaulu wa masomo yake ili kumwezesha kuendelea na masomo mwaka unaofuata au kwenda hatua nyingine ya masomo;
- Kwa mwanafunzi mnufaika ambaye anataka kuomba tena mkopo baada ya kusitisha masomo/chuo anatakiwa alipe angalau asilimia 25 ya fedha aliyoitumia kabla hajaomba mkopo mpya. Malipo ya 25% ya mkopo wa awali siyo dhamana ya kupangiwa mkopo;
VIGEZO VYA KUPATA MKOPO HESLB – BODI YA MIKOPO TANZANIA
(i) Mkopo utatolewa kwa kuzingatia uhitaji na programu;
(ii) Waombaji wapya ambao kwa sasa wanaendelea na masomo, lazima wawe wamehitimu elimu ya kidato cha sita (ACSEE) au stashahada (diploma) ndani ya miaka mitano, kuanzia mwaka 2020 hadi 2024.
(iii) Waombaji wote waliodahiliwa kusoma shahada mbalimbali kwa mwaka wa masomo 2024/2025 wanapaswa wawe wamehitimu kidato cha sita/Stashahada au sifa nyingine linganishi katika kipindi cha miaka mitano, yaani kati ya 2020 na 2024.