Kama wewe ni mwomba ajira katika Sekretarieti ya Ajira katika OR-Utumishi wa Umma, Basi hizi ndizo Sifa za Mwandishi Mwendesha Ofisi Katika Ajira Utumishi.
Mwandishi Mwendesha Ofisi ni mtu anayesimamia shughuli za kiutawala na kazi za ofisi kwa ufanisi. Majukumu yake ni pamoja na kupokea na kuelekeza simu, kupanga na kuhifadhi nyaraka, kuandaa mikutano na ratiba za ofisi, na kushughulikia mawasiliano ya barua pepe na barua za kawaida. Pia, anaweza kuwa na jukumu la kupokea wageni na kuhakikisha mazingira ya ofisi yanabaki safi na ya kuridhisha.
Kazi hii inahitaji ujuzi mzuri wa mawasiliano, uwezo wa kupanga kazi kwa ufanisi, na uelewa wa programu za kompyuta kama vile Microsoft Office. Mwandishi Mwendesha Ofisi ni kiungo muhimu kati ya wafanyakazi na usimamizi, akihakikisha kwamba shughuli za kila siku za ofisi zinafanyika kwa mpangilio na bila matatizo.
Sifa: Kuajiriwa Wahitimu wa Kidato cha Nne (Form Four) au Kidato cha Sita (Form Six) wenye Stashahada (Diploma) ya Uhazili au cheti cha NTA level 6 ya Uhazili. Aidha, wawe amefaulu somo la Hatimkato ya Kiswahili na Kiingereza maeneo 100 kwa dakika moja na kupata programu za kompyuta za ofisi kama vile: Word, Excel, Powepoint, Internet, E-mail na Publisher kutoka chuo chochote kinachotambuliwa na Serikali.
Mshahara wa Mwandishi Mwendesha Ofisi 2024/2025
Ni upi mshahara wa mtu aliesomea Maswala ya Mwandishi Mwendesha Ofisi?
Ngazi ya mshahara ni TGS C yaani Tshs. 585,000.00 na kuendelea kwa kila mwezi.