Tume ya Uchaguzi Tanzania wametangaza orodha ya majina ya walioitwa kwenye usaili NEC au INEC kwa mwezi huu julai 2024.
TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI
Afisa Mwandikishaji wa Jimbo la Nyang’hwale kwa mamlaka aliyopewa chini ya kifungu 12 (1) (C) cha kanuni za Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga kura za mwaka 2024, anapenda kuwaarifu waombaji wa nafasi za kazi za muda za Waandishi Wasaidizi na Waendeshaji wa Vifaa vya Bayometriki Waliouchaguliwa kufika kwenye usaili.
Usaili utafanyika Tarehe 22/07/2024 kwa tarafa za Msalala na Bukwimba, na Tarehe 23/07/2024 kwa tarafa za Nyang’hwale na Nyijundu kama ilivyoorodheshwa kwenye tangazo la kila Kata hapa chini.
Kila Msailiwa anatakiwa kuja na Kitambulisho kwa ajili ya utambuzi. Vitambulisho vinavyo kubalika ni pamoja na; Kitambulisho cha mpiga kura, Kitambulisho cha kazi, Kitambulisho cha uraia, Hati ya kusafiria, au reseni ya udereva.
Wasailiwa wanatakiwa kuja na VYETI VYAO HALISI (ORIGINAL CERTIFICATES) kuanzia cheti cha Kidato cha nne, Astashahada, Stashahada, Shahada na kuendelea kulingana na sifa/elimu ya muombaji.
Kila msailiwa atajigharamia kwa chakula, usafiri na malazi.
Kila Msailiwa azingatie tarehe, muda na mahali alipo pangiwa kufanyia usaili.
Orodha ya Majina ya walioitwa kwenye usaili yameorodheshwa hapa chini.
Limetolewa na;
Husna Toni Chambo
AFISA MWANDIKISHAJI (JIMBO)
NYANG’HWALE.
Orodha ya Majina ya kuitwa kwenye USAILI NEC.
Yatawekwa kwenye mbao za matangazo jimboni kwako au tembelea tovuti husika ya NEC/INEC