Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma anapenda kuwataarifu waombaji kazi wa nafasi mbalimbali waliofanya usaili kati ya tarehe 14-01-2023 na tarehe 21-06-2024 kuwa matokeo ya waombaji kazi waliofaulu usaili huo ni kama yalivyoorodheshwa katika tangazo hili. Orodha ya majina haya pia inajumuisha baadhi ya wasailiwa waliokuwa kwenye kanzidata (Database) kwa kada mbalimbali ambao wamepangiwa vituo vya kazi baada ya nafasi kupatikana.
Mamlaka ya Ajira
Shilika la Maendeleo la Taifa (NDC)
Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga
Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo
Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi
Halmashauri ya Mji wa Korogwe
Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na wenye Ulemavu
Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga
Halmashauri ya Manispaa ya Mtwara
Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga
Halmashauri ya Manispaa ya Temeke
Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni
Wizara ya Nishati
Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
Halmashauri ya Wilaya ya Kyela
Halmshauri ya Wilaya Karagwe
Bodi ya Waandisi (ERB)
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma
Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT)
Taasisi ya Maendeleo ya Jamii Tengeru (TICD)
Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH)
Bodi ya Huduma za Maktaba Tanzania (TLSB)
Waombaji waliofaulu usaili wanatakiwa kuchukua barua za kupangiwa kituo cha kazi katika Ofisi za Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma zilizopo katika Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) kwenye Majengo ya Dkt. Asha Rose Migiro, Masjala ya wazi ndani ya siku saba kutoka tarehe ya tangazo hili na baada ya hapo barua ambazo hazitachukuliwa na wahusika zitatumwa kupitia anuani zao za Posta.
Bonyeza hapa kudownload Tangazo la majina ya walioitwa kazini Utumishi
Orodha ya walioitwa kazini Utumishi 2024/2025.
Wanaokuja kuchukua barua za kupangiwa kituo cha kazi wanapaswa kuwa na kitambulisho kwa ajili ya utambuzi; Vitambulisho vinavyokubalika ni pamoja na:- Kitambulisho cha Uraia, Hati ya kusafiria, Kitambulisho cha Mzanzibari Mkaazi, Kitambulisho cha Mpiga kura au Leseni ya Udereva.
Kwa matangazo mbalimbali ya nafasi za kazi, ajira mpya kutoka serikalini tembelea https://ajira.go.tz.
Kuitwa kazini Utumishi 2024.
Pia, waombaji kazi waliofaulu usaili na kupangiwa kituo cha kazi wanatakiwa kuripoti kwa Mwajiri katika muda ambao umeainishwa kwenye barua za kupangiwa kituo cha kazi wakiwa na vyeti halisi (Originals Certificates) za masomo kuanzia kidato cha nne na kuendelea ili vihakikiwe na mwajiri kabla ya kupewa barua ya Ajira. Kwa wale ambao majina yao hayapo katika tangazo hili watambue kuwa hawakupata nafasi/hawakufaulu usaili, hivyo wasisite kuomba kwa mara nyingine nafasi za kazi zitakapotangazwa.
Endelea..