Leo kutoka INEC, Orodha ya majina ya Walioitwa kwenye Usaili INEC – Bukoba NEC; Afisa Mwandikishaji wa Jimbo la Bukoba Mjini anapenda kuwataarifu waombaji wote walioomba kazi ya Waandishi Wasaidizi na Waendeshaji wa Vifaa vya Bayometriki kuwa usaili unatarajiwa kuendeshwa tarehe 22 Julai, 2024 katika Ukumbi wa Shule ya Sekondari Ihungo saa 1:30 asubuhi.
Wasailiwa wanaoitwa kwenye usaili wanapaswa kuzingatia maelekezo yafuatayo:-
i. Usaili utafanyika tarehe 22 Julai, 2024 katika Ukumbi wa Shule ya Sekondari
Ihungo saa 1:30 asubuhi.
ii. Kila Msailiwa anapaswa kuwa na kitambulisho kwa ajili ya utambuzi.
iii. Vitambulisho vinavyokubalika ni pamoja na: Kitambulisho cha NIDA, Kitambulisho
cha Mpiga Kura, Kitambulisho cha Mkazi, Hati ya Kusafiria, Leseni ya Udereva, na
Barua ya Utambulisho toka Serikali ya Kijiji/Mtaa.
iv. Kila Msailiwa atajigharamia Chakula, Usafiri na Malazi.
v. Kila Msailiwa azingatie tarehe, muda na mahali alipopangiwa kufanyia usaili.
vi. Kila msailiwa aje na kalamu ya buluu au nyeusi kwa ajili ya usaili wa maandishi
vii. Waombaji kazi ambao majina yao hayakuonekana katika tangazo hili wasisite
kuomba tena pindi nafasi za kazi zitakapotangazwa na kuzingatia masharti ya
tangazo husika.
viii. Orodha ya wanaoitwa kwenye usaili imeambatanishwa na tangazo hii
Bonyeza hapa kudownload orodha ya majina ya walioitwa kwenye usaili INEC Bukoba
Uliza swali lolote hapo chini..
Orodha ya majina ya walioitwa kwenye usaili NEC – INEC mikoa mbalimbali
Tafadhali endelea kusubiri au tembelea kurasa la Tume ya Taifa ya Uchaguzi Tanzania