Karibu katika fursa mpya za ajira katika Wilaya ya Bumbuli kwa mwezi Julai 2024! Ikiwa na mazingira mazuri ya kazi na jamii yenye mshikamano, Bumbuli imetangaza Nafasi za kazi Wilaya ya Bumbuli – July 2024 | Ajira Mpya Bumbuli kwa wale wanaotafuta kuboresha maisha yao na kuchangia maendeleo ya eneo hili. Jiunge nasi kugundua nafasi hizi za ajira na kuanza safari yako ya kazi yenye mafanikio na fursa tele. Usikose nafasi hii ya kipekee ya kuwa sehemu ya mabadiliko na ukuaji wa Wilaya ya Bumbuli. Usikose kutembelea habaritimes.com, kwa makala mbalimbali ya nafasi za ajira zilizo tangazwa na serilaki mwezi huu.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Bumbuli amepokea kibali cha Ajira mpya kwa ikama ya mwaka 2023/2024 kutoka kwa Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora chenye Kumb.Na.FA.97/288/01/09 cha tarehe 25/06/2024. Hivyo Watanzania wote wenye sifa wanatangaziwa kutuma maombi ya kazi kwa nafasi zifuatazo:-
Ajira Portal chaneli | Jiunge hapa |
Nafasi za kazi zilizo tangazwa
1. Mtendaji wa Kijiji Daraja la III – Nafasi 20
Majukumu ya Mtendaji wa Kijiji:
- Kuwa Afisa masuhuli na Mtendaji Mkuu wa Serikali ya Kijiji;
- Kusimamia Ulinzi na Usalama wa raia na mali zao, kuwa mlinzi wa amani na msimamizi wa utawala bora katika Kijiji;
- Kuratibu na kusimamia upangaji wa utekelezaji wa mipango ya maendeleo ya Kijiji;
- Kuwa katibu wa mikutano na Kamati zote za Halmashauri ya Kijiji;
- Kutafsiri na kusimamia Sera, Sheria na Taratibu;
- Kuandaa taarifa za utekelezaji wa kazi katika eneo la kazi na kuhamasisha wananchi katika kuandaa na kutekeleza mikakati ya kuondoa njaa, umaskini na kuongeza uzalishaji mali;
- Kuwa kiongozi wa Wakuu wa Vitengo vya Kitaalam katika Kijiji;
- Kusimamia, kukusanya na kuhifadhi kumbukumbu zote na nyaraka za Kijiji;
- Kuwa Mwenyekiti wa kikao cha wataalamu katika Kijiji;
- Kusimamia utungaji wa sheria ndogo za Kijiji;
- Kupokea, kusikiliza na kutatua malalamiko na migogoro ya wananchi; na
- Atawajibika kwa Mtendaji wa Kata
Sifa za mwombaji:
Kuajiriwa mwenye elimu ya kidato cha nne/sita aliyehitimu mafunzo ya Astashahada/Cheti (NTA LEVEL 5) katika mojawapo ya fani zifuatazo: Utawala, Sheria Elimu ya Jamii, Usimamizi wa Fedha, Maendeleo ya Jamii na Sayansi ya sanaa kutoka vyuo vinavyotambuliwa na Serikali.
MSHAHARA: Kwa kuzingatia viwango vya mishahara ya serikali TGS B
2. Msaidizi wa Kumbukumbu Daraja la II – Nafasi 4
Majukumu ya Msaidizi wa Kumbukumbu:
- Kuorodhesha barua zinazoingia masjala;
- Kuorodhesha barua zinazotoka nje ya Taasisi (Outgoing Correspondence Register);
- Kusambaza majalada kwa watendaji (Action Officers);
- Kupokea majalada yanayorudi masjala kutoka kwa watendaji;
- Kutafuta kumbukumbu/Nyaraka au majalada yanayohitajika na watendaji;
- Kurudisha majalada kwenye shubaka/kabati la majalada (Racks/Filling Cabinets) au Mahali Pengine yanapohifadhiwa; na
- Kufuatilia mzunguko wa majalada ndani nan je ya Taasisi (File tracking).
Sifa za Msaidizi wa Kumbukumbu:
Awe amehitimu Elimu ya Kidato cha Nne (IV) au Kidato cha Sita (VI) aliyehitimu Stashahada (NTA level 6) katika fani ya Masjala kutoka Vyuo vinavyotambuliwa na Serikali, mwenye ujuzi wa Kompyuta.
NGAZI YA MSHAHARA
- Kwa kuzingatia ngazi za mishahara ya Serikali – TGS C
3. Mwandishi Mwendesha Ofisi II – Nafasi 3
Sifa za Mwombaji;
Awe amefaulu Kidato cha Nne (IV) au kidato cha Sita (VI) wenye Stashahada (Diploma) ya Uhazili au Cheti cha NTA level 6 ya Uhazili. Aidha awe amefaulu somo la Hatimkato ya Kiswahili na Kiingereza maneno 100 kwa dakika moja na kupata programu za compyuta za ofisi kama vile: – Word,Excel, Power point, Internet, E-mail na Publisher kutoka chuo chochote kinachotambuliwa na Serikali
KAZI NA MAJUKUMU:
- Kuchapa barua, taarifa na nyaraka za kawaida na za Siri;
- Kupokea wageni na kuwasili shida zao na kuwaeleza wanapoweza kusaidiwa;
- Kutunza taarifa za kumbukumbu ya matuokio, miadi, tarehe za vikao, safari za Mkuu wake na ratiba za kazi zingine;
- Kutafuta majalada na nyaraka zinazohitajika katika utekelezaji wajukumu ya kazi;
- Kupokea majalada na kusambaza kwa maofisa walio katika Idara/Kitengo/Sehemu husika;
- Kukusanya, kutunza na kuyarejesha majalada na nyaraka sehemu zinahusika;
- Kupanga dondoo na kufanya maandalizi ya vikao mbalimbali;
- Kuandaa orodha ya mahitaji ya vifaa vya Ofisi; na
NGAZI YA MSHAHARA: Kwa kuzingatia ngazi za mishahara ya Serikali – TGS C
4. Dereva Daraja la II – Nafasi 4
MAJUKUMU YA KAZI:
- Kukagua gari kabla na baada ya safari ili kubaini hali ya usalama wa gari;
- Kuwapeleka Watumishi maeneo mbalimbali kwenye safari za kikazi;
- Kufanya matengenezo madogo madogo ya gari;
- Kutunza na kuandika daftari la safari “log book” kwa safari zote. V. Kukusanya na kusambaza nyaraka mbalimbali;
- Kufanya usafi wa Gari; na
- Kufanya kazi nyingine kadri atakavyoelekezwa na Msimamizi wake.
SIFA ZA MWOMBAJI;
Awe na cheti cha Mtihani wa Kidato cha Nne (IV), mwenye leseni Daraja ‘E’ au ‘C’ ya uendeshaji pamoja na uzoefu wa kuendesha magari kwa muda usiopungua Mwaka mmoja (1) bila kusababisha ajali, Awe amehudhuria mafunzo ya msingi ya Uendeshaji Magari (Basic Driving Course) yanayotolewa na chuo cha Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) au Chuo kingine kinachotambuliwa na Serikali
NGAZI YA MSHAHARA Kwa kuzingatia viwango vya Serikali TGS B.
Leave a comment