Leo kutoka Utumishi, Jinsi ya kubadili taarifa ajiraportal – Jinsi ya kufuta cheti, document yoyote ile Jinsi ya kuedit / kurekebisha nakala Ajira Portal; Ofisi ya Rais, Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma ilianzishwa kwa mujibu wa kifungu 29 (1) cha Sheria ya Utumishi wa Umma, Sura ya 298 iliyorejewa 2019, ambayo inaelekeza kuwepo kwa chombo maalumu cha kushughulikia mchakato wa Ajira katika Utumishi wa Umma.
Jukumu la msingi la Ofisi ya Rais, Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma ni kuwezesha mchakato wa ajira katika Utumishi wa Umma kwa kushirikiana na Idara na Taasisi mbalimbali za Umma.
Hivi karibuni zimetangazwa nafasi za kazi mbalimbali na watanzania wenye sifa wanatakiwa kuomba nafasi hizo kupitia mfumo wa Ajira Portal. Katika mfumo huu muombaji kazi anatakiwa kupakia nakala za vyeti vyake ambazo zimehakikiwa na kugongwa mhuri na Mwanasheria au Wakili kuonesha kuwa ni nakala kutoka katika vyeti halisi.
Pia Muomba kazi anatakiwa kupakia vyeti vyake kwenye mfumo kulingana na kiwango chake cha elimu ili kumuwezesha kuomba pindi nafasi zinapo tangazwa. Ikitokea umeudanganya mfumo au umeweka cheti cha taaluma kisicho cha kwako, au unataka kuomba nafasi ya juu au ya chini kulinganisha na cheti cha taaluma ulichonacho, hutoweza kuomba nafasi uliyoomba kwani mfumo unamtambua cheti chako cha elimu ambacho umeweka kwenye mfumo.
Ikitokea umekosea kupakia cheti chako, Mfumo hauto kuruhusu kufuta cheti chako bali utalazimika kwenda sehemu uliyo kosea na kuhariri (edit) cheti chako kisha kupakia (upload) kilicho sahihi.
Hata hivyo; Ofisi ya Rais, Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma imetambua changamoto wanazokutana nazo waombaji kazi na imeweka simu ya Huduma kwa mteja namba 0262160350 inayopatikana kuanzia saa 2.00 Asubuhi mpaka saa 12.00 Jioni kwa siku za kazi na Maafisa wapo tayari kwa ajili ya kutoa huduma au unaweza kutuma barua kupitia ict@ajira.go.tz.
Jinsi ya kubadili Taarifa katika Mfumo wa Ajira Portal Utumishi.
Pia kwa Msaada zaidi unaweza kufika katika Ofisi zetu zilizopo Dodoma katika majengo ya Dr. Asha Rose Migiro, Dar es Salaam – Magogoni, na Zanzibar – Mazizini (Jengo la sheria, Ghorofa ya tatu) kwa ajili ya msaada zaidi.
Aidha, tunawasihi waomba kazi kujaza taarifa na kupakia nakala za vyeti vyao kwenye mfumo wa Ajira portal wao wenyewe na si kufanyiwa na mtu mwingine ili kuepuka makosa yanayoweza kuepukika, na pia mnatakiwa kuzingatia taratibu na masharti yaliyoekwa kwani watanzania wengi wameweza kuomba kazi na kufanikiwa.
Epuka Matapeli, soma maelekezo kabla ya kupakia vyeti vyako na kuomba nafasi ya kazi uliyo kusudia.
Lynn Chawala
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
Je ni lazima vyeti vipigwe mhuri na mwanasheria kwa sisi walimu wa grade IIIA
Binafsi nimekubwa na hiyo Changamoto lakini shida ni kwamba Simu haizipokelewi na wengine Tuko Mbali na Dodoma Nimepiga Simu Dakika Arobain na Tano Zimekatika lakin Simu yangu haikupokelewa
Habari mkuu,
Mimi naona hujasoma maelezo kila kitu kimeandikwa hapo jinsi ya kutatua changamoto yako.
Kuna namba za huduma kwa wateja utumishi pia email ya kuwasiliana na kitengo cha utumishi (ICT).
Unatakiwankuwa na subira hadi simu itakapopokelewa, unaeza subiri hadi dk 45 ndipo inapokelewa.
Inachelewa kuoikelewa kwasababu yakuwepo kwa wateja wengi wenye changamoto kama zakwako.
Hivyo, unapopiga simu, usikate, subiri hadi itakapo pokelewa.
Jinsi ya kufuta cheti
Samahani naomba msaada wa kufuta vyeti cha diploma n certificte nlivyoapload kimakosa
Habari? namna ya kufuta cheti katika kipengele cha academic qualification
hii ni changamoto kwa wengi
tunaopmba msaada namna ya kufuta cheti maana maelekezo mnayotoa kuedit lakin kweny program haileti