Leo kutoka utumishi, Ajira mpya Nafasi za kazi Igunga; Mkurugenzi amepata kibali kipya cha ajira kwa ikama ya mwaka 2023/2024 chenye Kumb. Na. FA. 97/288/01/09 cha tarehe 25.06.2024 kutoka kwa Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora. Kufuatia kibali hicho Mkurugenzi wa Halmashauri ya Igunga anakaribisha maombi kwa watanzania wenye sifa za kujaza nafasi za kazi zifuatazo :-
Nafasi zilizo Tangazwa Igunga
- MTENDAJI WA KIJIJI III – NAFASI (15)
- MSAIDIZI WA KUMBUKUMBU DARAJA II – NAFASI (05)
- DEREVA DARAJA LA II – NAFASI (05)
Bonyeza hapa kudownload Tangazo la nafasi za kazi Igunga
Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania na wenye umri wa kuanzia miaka 18 na usiozidi miaka 45 isipokuwa kwa wale tu walioko kazini serikalini.
Waombaji wote waambatishe cheti cha kuzaliwa kilichothibitishwa na Mwanasheria/Wakili.
Endelea kusoma maelezo chini.
Ajira Mpya Igunga – Nafasi za Halmashauri Utumishi 2024.
Mwisho wa kutuma maombi ni tarehe 31 Julai, 2024.
MUHIMU: Kumbuka kuambatisha barua yako ya maombi ya kazi
iliyosainiwapamoja na vyeti vya elimu, Anuani ya barua hiyo ielekezwe kwa;
MKURUGENZI MTENDAJI,
HALMASHAURI YA WILAYA YA IGUNGA,
S.L.P. 19,
IGUNGA.