Leo kutoka utumishi (PSRS), Ajira Mpya – Nafasi za kazi Kigamboni – Utumishi 2024; Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni anawatangazia Watanzania wenye sifa na nia ya kufanya kazi katika Manispaa ya Kigamboni kuomba nafasi za kazi ziliyotajwa hapo chini, baada ya kupokea kibali chenye Kumb. Na. FA.97/288/01/09 cha tarehe 25 Juni, 2024 kutoka kwa Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora.
Ajira Mpya Kigamboni
DEREVA II – NAFASI 5: Leseni ya Daraja la āEā au āCā ya uendeshaji magari ambayo amefanyia kazi kwa muda usiopungua mwaka mmoja bila kusababisha ajali na awe amehudhuria mafunzo ya Msingi ya uendeshaji Magari
WASAIDIZI WA KUMBUKUMBU II – NAFASI 10: Awe na Elimu ya kidato cha Nne (Form IV) au cha Sita (Form VI) aliehitimu mafunzo ya Stashahada /Diploma (NTA Level 6) katika fani ya utunzaji wa kumbukumbu kutoka vyuo vinavyotambuliwa na Serikali, wenye ujuzi wa kompyuta.
Bonyeza hapa kudownload Tangazo la nafasi za kazi Kigamboni
Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania na wenye umri wa kuanzia miaka 18 na usiozidi miaka 45 isipokuwa kwa wale tu walioko kazini Serikalini.
Ajira Mpya Kigamboni – Nafasi za Halmashauri 2024 Utumishi.
Waombaji ambao tayari ni watumishi wa Umma na wamejipatia sifa za kungilia kazi kwa waajiri wao na waajiri wajiridhishe ipasavyo.
Mwisho wa kupokea maombi ya kazi ni tarehe 27.07.2024.
MUHIMU: Kumbuka kuambatisha barua yako ya maombi ya kazi iliosainishwa pamoja na vyeti vya Elimu. Anuani ya barua hiyoielekezwe kwa: –
Mkurugenzi wa Manispaa,
Halmashauri ya Manispaa Kigamboni,
S.L.P. 36009,
Kigamboni – Dar Es Salaam.
Jinsi ya kutumia maombi nimeshindwa ila jinsi ya kutunza records naweza ila naomba kusaidiwa jinsi ya kutuma maombi šš
Jinsi ya kutuma maombi katika nafasi za kazi Kigamboni 2024 Utumishi.
Maombi yote ya kazi yatumwe kwenye mfumo wa kielektroniki wa ajira (Recruitment Portal) kupitia anuani ifuatayo https://portal.ajira.go.tz, aidha hakuna maombi yatakayopokelewa kwa njia tofauti na iliyotajwa.
Limetolewa Na: –
E. N. Kiwale
Mkurugenzi Manispaa ya Kigamboni.