Sekretarieti ya Ajita; Leo Serikali kupitia PSRS imetangaza ajira mpya katika Nafasi za Kazi Wilaya ya Mtama – Utumishi Julai 2024. Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mtama amepokea kibali cha Ajira mpya kwa ikama ya mwaka 2023/2024 kutoka kwa Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora chenye Kumb. Na. FA.97/288/01/09 cha tarehe 25/06/2024. Hivyo Watanzania wote wenye sifa wanatangaziwa kutuma maombi ya kazi kwa nafasi zifuatazo:
Kumb. Na MDC/M.13/28/VOL.I/132
Ajira Mpya Mtama
1. MTENDAJI WA KIJIJI DARAJA LA III – NAFASI 20
2. DEREVA DARAJA LA II – NAFASI 7
3. MWANDISHI MWENDESHA OFISI DARAJA LA II – NAFASI 8
4. MSAIDIZI WA KUMBUKUMBU DARAJA LA II – NAFASI 4
Maombi yote yaambatane na vyeti vya Elimu na Taaluma vilivyothibitishwa na Mwanasheria/Wakili ambavyo ni vyeti vya Kidato cha Nne au Sita kwa wale waliofikia kiwango hicho na Vyeti vya kuhitimu mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi husika.
Ajira Mpya Mtama 2024
Mwisho wa kutuma maombi ni tarehe 04 Agosti 2024
MUHIMU: Kumbuka kuambatanisha barua yako ya maombi ya kazi iliyosainiwa pamoja nav yeti vya elimu, anuani ya barua hiyo ielekezwe kwa:-
MKURUGENZI MTENDAJI WA HALMASHAURI
HALMASHAURI YA WILAYA YA MTAMA
S.L.P 328
MTAMA