Leo hii hapa orodha ya Majina ya Walioitwa kwenye Usaili Polisi Aprili 23, 2025 – Tanzania TPF. Mkuu wa Jeshi la Polisi anapenda kuwatangazia kuwa vijana walioomba ajira ya Jeshi la Polisi kupitia mfumo wa Ajira TANZANIA POLICE FORCE RECRUITMENT PORTAL, usaili wao utafanyika kuanzia tarehe 28/4/2025 hadi tarehe 11/5/2025 kote nchini.
Kwa wasailiwa wenye elimu ya Shahada, Stashahada na Astashahada usaili utafanyika jijini Dar es Salaam katika uwanja wa gwaride uliopo Kambi ya Polisi (Police Barracks) barabara ya Kilwa nyuma ya kituo cha Polisi Kilwa Road.
Ajira Chaneli | Jiunge hapa |

Bonyeza hapa kupakua pdf ya majina
Kila msailiwa atalazimika kufika eneo la usaili akiwa na vyeti halisi vya taaluma (Academic certificates), cheti cha kuzaliwa, kitambulisho cha Taifa cha NIDA au namba ya NIDA pamoja na nguo na viatu vya michezo. Msailiwa atakayefika kwenye usaili baada ya tarehe 28/04/2025 hatapokelewa. Aidha, orodha ya waliochaguliwa kufanya usaili imeambatishwa pamoja na tangazo hili.
Pia, Kwa wasailiwa wa Zanzibar wenye elimu ya Shahada, Stashahada, Astashahada, Kidato cha sita na Nne, usaili utafanyika Zanzibar ambapo kwa walioko mikoa ya Unguja, usaili utafanyika Makao Makuu ya Polisi Zanzibar (Ziwani) na Mikoa ya Pemba usaili utafanyika Ofisi ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kusini Pemba (Chakechake).
Endelea kusoma baadhi ya maelezo chni hapa kwa ajili ya usaili.
KUITWA KWENYE USAILI JESHI LA POLISI TANZANIA 2024.
Waombaji wenye elimu ya kidato cha nne na sita usaili wao utafanyika kwenye
mikoa walioichagua wakati wa kutuma maombi.
Unayapataje majin
Majina tunayapataje
Je na nguo za michezo tunaenda nazo pair ngap na tunakaa kama kambi au ni kuja na kurudi