Leo, sekretarieti ya ajira imetangaza orodha ya majina ya Walioitwa kwenye Usaili Bunge la Tanzania PDF – Utumishi Agosti 2024. Katibu wa Bunge anapenda kuwataarifu Waombaji Kazi wote walioomba kazi katika Utumishi wa Bunge kuwa, usaili unatarajiwa kufanyika kuanzia tarehe 24-08-2024 hadi 29-08-2024 Jijini Dodoma. Wasailiwa walioitwa kwenye usaili wanapaswa kuzingatia maelekezo yafuatayo:-
Kuitwa kwenye Usaili Bunge la Tanzania
RATIBA YA USAILI WA MCHUJO
MWAJIRI | KADA | TAREHE YA USAILI | MAHALI | |
Bunge | AFISA TAWALA DARAJA LA II | 24-08-2024 07:00 AM | UNIVERSITY OF DODOMA, COLLEGE OF INFORMATION AND VIRTUAL EDUCATION (CIVE), AUDITORIUM HALL | |
Bunge | FUNDI SANIFU DARAJA LA II (UMEME) | 24-08-2024 07:00 AM | UNIVERSITY OF DODOMA, COLLEGE OF BUSINESS EDUCATION (COBE)CBSL 1 | |
Bunge | MTEKNOLOJIA DAWA DARAJA LA II | 24-08-2024 07:00 AM | UNIVERSITY OF DODOMA, COLLEGE OF BUSINESS EDUCATION (COBE)CBSL 2 | |
Bunge | FUNDI SANIFU DARAJA LA II (UFUNDI) | 24-08-2024 07:00 AM | UNIVERSITY OF DODOMA, COLLEGE OF BUSINESS EDUCATION (COBE)CBSL 1 | |
Bunge | TABIBU WA KINYWA NA MENO DARAJA LA II (DENTAL THERAPIST) | 24-08-2024 07:00 AM | UNIVERSITY OF DODOMA, COLLEGE OF BUSINESS EDUCATION (COBE)CBSL 1 |
RATIBA YA USAILI WA VITENDO
MWAJIRI | KADA | TAREHE YA USAILI | MAHALI | |
Bunge | FUNDI SANIFU DARAJA LA II (UMEME) | 26-08-2024 08:00 AM | CHUO CHA UFUNDI VETA, DODOMA | |
Bunge | FUNDI SANIFU DARAJA LA II (UFUNDI) | 26-08-2024 08:00 AM | CHUO CHA UFUNDI VETA, DODOMA |
RATIBA YA USAILI WA MAHOJIANO
MWAJIRI | KADA | TAREHE YA USAILI | MAHALI | |
Bunge | AFISA TAWALA DARAJA LA II | 28-08-2024 07:30 AM | OFISI YA BUNGE – DODOMA, JENGO LA UTAWALA, GHOROFA YA TANO | |
Bunge | FUNDI SANIFU DARAJA LA II (UMEME) | 29-08-2024 07:30 AM | OFISI YA BUNGE – DODOMA , JENGO LA UTAWALA, GHOROFA YA TANO | |
Bunge | MTEKNOLOJIA DAWA DARAJA LA II | 28-08-2024 07:30 AM | OFISI YA BUNGE – DODOMA , JENGO LA UTAWALA, GHOROFA YA TANO | |
Bunge | FUNDI SANIFU DARAJA LA II (UFUNDI) | 29-08-2024 07:30 AM | OFISI YA BUNGE – DODOMA , JENGO LA UTAWALA, GHOROFA YA TANO | |
Bunge | TABIBU WA KINYWA NA MENO DARAJA LA II (DENTAL THERAPIST) | 28-08-2024 07:30 AM | OFISI YA BUNGE – DODOMA , JENGO LA UTAWALA, GHOROFA YA TANO |
Bonyeza hapa kudownload tangazo la walioitwa kwenye usaili Bunge la Tanzania
KUITWA KWENYE USAILI BUNGE LA TANZANIA – UTUMISHI (PSRS)
1. Usaili wa Mchujo utafanyika kama ilivyooneshwa kwenye tangazo hili. Muda na mahali ambapo usaili utafanyika umeainishwa kwa kila Kada.
2. Kila Msailiwa anatakiwa kufika akiwa amevaa NADHIFU.
3. Kila Msailiwa anapaswa kuwa na kitambulisho kwa ajili ya utambuzi. Vitambulisho vinavyokubalika ni pamoja na:- Kitambulisho cha Mkazi, Kitambulisho cha Mpiga kura, Kitambulisho cha kazi, Kitambulisho cha Uraia au Hati ya kusafiria.
4. Wasailiwa wanatakiwa kufika na VYETI VYAO HALISI (ORIGINAL), kuanzia cheti cha kuzaliwa, kidato cha IV, VI, Stashahada, Stashahada ya Juu, Shahada na kuendelea kutegemeana na sifa za Mwombaji.
5. Wasailiwa watakaowasilisha (Testimonials, Provisional Results, Statement of results) hati za matokeo HAZITAKUBALIWA NA HAWATARUHUSIWA KUENDELEA NA USAILI.
ORODHA YA MAJINA YA WALIOITWA KWENYE USAILI BUNGE LA TANZANIA UTUMISHI AGOSTI 2024
1. Kila Msailiwa atajigharamia kwa Chakula, Usafiri na Malazi.
2. Kila Msailiwa azingatie tarehe, muda na mahali alipopangiwa kufanyia usaili.
3. Kwa waombaji waliosoma nje ya Tanzania wanatakiwa kufika na Hati za Uhakiki wa Vyeti vyao kutoka kwa Mamlaka zinazohusika (kama TCU, NACTE au NECTA)
4. Waombaji kazi ambao majina yao hayakuonekana katika tangazo hili watambue kuwa hawakukidhi vigezo. Hivyo, wasisite kuomba tena pindi nafasi za kazi zitakapotangazwa kwa kuzingatia mahitaji ya tangazo husika.
5. Kwa kada ambazo wanatakiwa kusajiliwa na Bodi zao za Kitaaluma wanapaswa kuja na vyeti vyao Halisi vya Usajili pamoja na Leseni za kufanyia kazi.
6. Wasailiwa wote walioitwa kwenye usaili wahakikishe wanaingia kwenye akaunti zao na kunakili namba ya mtihani kwa kuwa namba hizo hazitatolewa siku ya usaili
7. Wasailiwa wote mnajulishwa kuwa kwa sasa, hali ya hewa ya Jiji la Dodoma ni baridi hivyo mnashauriwa kuvaa nguo zinazohimili hali ya hewa ya ubaridi.